Sunday, January 13, 2013

Tangazo kwa wanachama wa jumuhiya ya wa Tanzania DMV



Tunapenda kuwatangazia kuwa wale wote ambao ni wanachama wa jumuiya ya watanzania DMV mnaweza kuona Members Area page kwenye mtandao wetu wa jumuiya. Members Area page ina vitu ambavyo vinawahusu ACTIVE members only, kama vile financial report, list of active members, na vitu kama hivyo.

Kama wewe ni active member na unahitaji kutembelea Members Area page tafadhali fanya ifuatavyo (kwenye komputa au simu yako):
- Tembelea www.watanzaniadmv.org

- Bofya ukurasa wa Members Area
- Kwa sababu hauna password, bofya “Forgot your password ? click here
- Weka email address yako, halafu nenda kwenye email yako utapata password yako.
- Ukipata ujumbe kuwa email address yako haipo kwenye database yetu, basi kwa maana hiyo email unayotumia hatunayo, na itabidi ufuate maelezo hapo chini.
- Njoo tena kwenye ukurasa wa Members Area, tumia hiyo password ku login kwenye ukurasa huu na endelea ku enjoy!.

Tahadhali: Email zinazofanya kazi ni zile tu ambazo tunazo kwenye database yetu, kama umebadilisha email au bado haujatupatia email yako, tafadhali tutumie jina lako kamili, address yako, email yako na namba yako ya simu (Tutakupigia simu ili kuhakikisha “identity” yako). Tuma email yako kwa webmaster@watanzaniadmv.org, vile vile unaweza kuwapigia viongozi wa jumuhiya. Contact zao zinapatikana hapa: http://watanzaniadmv.org/contact.asp.


Ahsanteni sana,

Watanzania DMV

No comments:

Post a Comment