Monday, October 20, 2014

Mama Salma Kikwete Atunukiwa kwa Juhudi zake za Kupambana na Saratani ya Matiti


Mama Salma Kikwete Jumamosi Tarehe 18. 2014 alitunukiwa tuzo ya juhudi zake anazozifanya za kupambana na Saratani ya Matiti. Tuzo hiyo ilitolewa na taasisi ya African Women's Cancer Awareness Assocition kwenye hafla ya Gala Dinner iliyofanyika kwenye hoteli ya Omni Shoreham Hotel iyopo Washington DC.

Balozi Liberata Mulamula Akikabidhiwa Tuzo hiyo kwa Niaba ya Mama Salma Kikwete na Rais Wa African Women's Cancer Association Ms. Ify Anne Nwabukwu, RN, BSN
Muheshimiwa balozi akinyanyuwa Tuzo hiyo juu na Kusema " This is For Tanzania"


Balozi wa Marekani Mh. Liberata Mulamula akitoa risala fupi kwa niaba ya Mama Salma Kikwete kwenye Hafla hiyo.

Rais wa Jumuiya Bwana Iddi Sandaly, na Wawakilishi wa tano Ladies Asha Nyanganyi na Asha Harizi, wakiwa na Wana DMV mbali mbali ambao ni Wadau wa Maswala ya Saratani walioudhuria kwenye Gala Dinner hiyo iliyotowa tuzo pamoja na kutahimin  athari na mpambano wa Saratani ya Matiti.  
Mtangazaji wa Fox 5 Channel Maureen Umeh ambaye alikuwa ndie MC

Tano Ladies wakiwa na Rais wa African Women's Cancer Association Ms. Ify Anne Nwabukwu, RN, BSN. Tano Ladies wamekuwa wakishirikiana kwa karibu sana na Taasisi hii , ni ushirikiano wao ulioleta matunda kwa Taasisi hii kuweza kumkabidhi Mama Salma kikwete kipimo cha Mammogram ili kiende Tanzania.



































No comments:

Post a Comment