Saturday, November 2, 2013

The late Special Force Comando Lt. Rajab Mlima.

Watanzania Washington  DC Wamuombea Dua  Luteni Rajab Mlima   Mamia ya Watanzania wa DMV area leo wakiongozwa  na Mwenyekiti wa Jumuia ya Watanzania, akimkaribisha Mgeni Rasmi kutoka Ubalozini na Watanzania wote waliobahatika kuhudhuria kwenye kisomo.

 kwenye Ukumbi wa 11901 Claridge road Wheaton MD 201902 pamoja  na Military Attache  Kanali Mutta



Mwakilishi wa Balozi  akitoa Machache picha ya juu.
 kumombea Marehemu Kamanda Rajabu Mlima aliezaliwa August 30 1977 na Kuuwawa October 27 ,2013

Watu wakipata rakaa wakti wa sala na baadae kuendelea na kisomo cha kumuombea marehemu.





****************************
 Kumbu kumbu na Majonzi ! Mchumba wa Luteni Mlima akimliwaza mtoto wa marehemu aliefika kutoa heshima za Mwisho za Baba yake  huko Dar Juzi.


Mchumba wa askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), aliyeuawa kwa kupigwa risasi akiwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Luteni Asia Hussein aliyekuwa naye kabla ya kuuawa mchumba wake amesema, marehemu alimwomba amwombee arudi salama kutoka kwenye mapigano.
Pia, alisema kauli hiyo ndiyo ya mwisho kuisikia kutoka kinywani mwa mchumba wake huyo aliitoa baada ya kutolewa amri ya kijeshi kwamba anatakiwa kwenda kuwasaidia wenzake waliokuwa kwenye mapigano na askari wa waasi wa M23.
Askari huyo wa(JWTZ), Luteni Rajab Ahmed Mlima, aliuawa akiwa kwenye uwanja wa mapambano na vikosi vya askari wa waasi wa M23 katika milima ya Gavana, karibu na Goma, DRC wakati akitekeleza jukumu la ulinzi wa amani.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili jana nyumbani kwake, Luteni Asia alisema, “Ninachokumbuka walitakiwa kwenda kuwasaidia wenzao waliokuwa kwenye mapigano kwa muda mrefu, tayari walikuwa wamezidiwa nguvu na askari wa waasi wa M23, ukweli hali ilikuwa mbaya na mimi nilimkataza asiende kwa kuhofia usalama wake,” alisema Luteni Asia huku akibubujikwa machozi.
Alisema wakati akimsihi asiende alimjibu kwamba ni lazima aende kuwasaidia wenzao, kwani kazi waliyotumwa kuifanya ni pamoja na hiyo hivyo asingeweza kuacha kwenda.
Aidha, Luteni Hussein alibainisha kuwa baada ya kwenda kutoa msaada na kufanikiwa kuwadhibiti waasi, muda mfupi baadaye alipata taarifa kuwa Luteni Mlima amefariki kwa kupigwa risasi jambo lililomshtua kiasi cha kuishiwa nguvu kabisa.Kusoma zaidi bofya
Alisema kwa kuwa kazi ya Mungu haina makosa, yeye anamwombea huko aliko apumzike kwa amani kwani amefariki akiwa anawatetea wananchi wa DRC na kuiwakilisha nchi yake.
Mipango ya harusi
Akielezea mipango yao ya harusi, Luteni Asia alisema Desemba 28, mwaka huu walipanga kufunga ndoa na kwamba taratibu zote zilikuwa zimekamilika ikiwa pamoja kutolewa mahari.
“Kwa kweli jambo linalo niuma sana na siwezi kusahau ni kwamba, tulikuwa tumebakiza muda mfupi tufunge ndoa na kila kitu kilikuwa kimeshakamilika hadi ukumbi wa kufanyia sherehe ya harusi yetu tulishaulipia,” alisema Luteni Hussein huku akibubujikwa na machozi.

Portrait of the fallen soldier Lt. Rajab Ahmed Mlima


  He lost his life for the values of the United Nations, for protecting civilians, for defending human rights, for fighting for the benefit of the Democratic Republic of the Congo."
Message from UN Secretary-General Ban Ki-moon's Special Representative for the Democratic Republic of the Congo travelled to Kiwanja from Goma on Monday (28 Oct) to officiate a memorial service for the Tanzanian soldier killed recently in Rutshuru. Kiwanja is situated 70 km north of Goma, the capital of the North Kivu province of the DRC. Martin Kobler, who is also the Head of the United Nations Organization Stabilization Mission in the Democratic Republic of the Congo (MONUSCO) presided over the ceremony. He paid tribute to the fallen soldier, Lt. Rajab Ahmed Mlima, who died in line of duty while fighting the M23 rebels. Several other soldiers were also injured in the fight. The soldier from the Tanzanian Special Forces was part of the Intervention Force Brigade (IFB) that was formed to disarm armed groups in the North Kivu province. Fighting between the Congolese army the FARDC and M23 rebels resumed last week in the area known as Kibumba, 20 km from Goma. In recent days, the M23 rebels have lost key positions like Kibumba, Kiwanja, Rutshuru and Rumangabo.

1 comment: