Thursday, August 14, 2014

HEALTH FAIR & BAZAAR


BBQ YA WATANZANIA WOTE DMV - THIS SATURDAY


Ndugu Wana DMV. Wote Mnaombwa na Kukaribishwa kwenye COOKOUT (BBQ) ya Pamoja ya Watanzania wote wa Hapa DMV. 
Watoto, Wazee na Vijana 

Jumamosi Hii August 16, 2014
Lengo ni kukutana watanzania wote, kufahamiana, kujadiliana, Ku Network na kushauriana na kuimarisha , udugu, upendo, amani na umoja wetu.


Tunawaomba Wote Muudhurie.

HII NI BBQ YA JUMUIYA NA WOTE TUNAKARIBISHWA NA TUNAOMBWA TUUDHURIE.

BBQ hii itafanyika:


1030 Forest Glen Road

Silver Spring, MD 20901


Kuanzia 5:00 PM- Mpaka 9PM




Wednesday, November 13, 2013

NAFASI ZA KAZI - By The Association of Tanzanian Community in DMV - With a Big Language Institution in Washington DC



The Association of Tanzanian Community in DMV is announcing to the ACTIVE members only, that there is an immediate need for a Swahili Curriculum Developer for a 6-8 month project with a Big Language Institution in Washington DC . Hours would be full-time, and start date ASAP.
 
Please let us know if you are personally interested .
 
Basic requirements for the successful candidate are:
                -1-2 years of experience developing curriculum, preferably for adult learners or 1-2 years of adult instruction experience
                -Must be educated native speakers of Swahili and possess a university degree
                -Applicants must provide proof of eligibility to work in the US without sponsorship
 
For more information please call DMV leaders. Contacts are available at www.watanzaniadmv.org  or email us at info@watanzaniadmv.org
 
 
 IMETOLEWA NA UONGOZI
Jumuiya ya Watanzania DMV

Sunday, November 10, 2013

MAKARIBISHO YA BALOZI MPYA WASHINGTON DC




Rais wa Jumuia ya DMV akifungua Mkutano kumkaribisha Balozi



VIONGOZI WA JUMUIA JUU WAKIMKARIBISHA BALOZI MPYA


Balozi akiwa amekaa kwenye mezaa kuu.

BALOZI akitoa hotuba yake ya kutaka Watanzania kushikamana kuiimarisha Jumuia yao na kulipia unachama  na kutoa michango yeye akiwa Mwanachama mpya pia 

Wanachama wakimsikiliza Balozi mpya.


Mwenyekiti wa Zanzibar Diaspora  Omar Ally akitoa salamu kwa Wana jumuia.


Friends of Tanzania Association akitoa salamu zao



Kiongozi wa Southern community  akijitambulisha kwa Watanzaia 

BALOZI AKIWA NA  WATANZANIA 


Raisi wa DMV , Balozi na Mwenyekiti wa Diaspora .

 Balozi Mpya na Mshereheshaji wa shughuli Sunday Shomari

Mr charahani akiangalia utaratibu wa vinywaji.


DIDI VAVA AKIFANYA VITU VYAKE KWENYE CORNER  YA VINYWAJI


MAKULATI YA KUMWAGA  JUMUIA ILIJITAYARISHA VYA KUTOSHA



Balozi akilishwa keki na Rais wa Watanzania 


Balozi akicheza muziki kufurahia na Wanajumuia .


Mh. Balozi Mulamula alipokutana na uongozi wa jumuiya ya watanzania DMV Mwezi wa October.








Saturday, November 2, 2013

The late Special Force Comando Lt. Rajab Mlima.

Watanzania Washington  DC Wamuombea Dua  Luteni Rajab Mlima   Mamia ya Watanzania wa DMV area leo wakiongozwa  na Mwenyekiti wa Jumuia ya Watanzania, akimkaribisha Mgeni Rasmi kutoka Ubalozini na Watanzania wote waliobahatika kuhudhuria kwenye kisomo.

 kwenye Ukumbi wa 11901 Claridge road Wheaton MD 201902 pamoja  na Military Attache  Kanali Mutta



Mwakilishi wa Balozi  akitoa Machache picha ya juu.
 kumombea Marehemu Kamanda Rajabu Mlima aliezaliwa August 30 1977 na Kuuwawa October 27 ,2013

Watu wakipata rakaa wakti wa sala na baadae kuendelea na kisomo cha kumuombea marehemu.





****************************
 Kumbu kumbu na Majonzi ! Mchumba wa Luteni Mlima akimliwaza mtoto wa marehemu aliefika kutoa heshima za Mwisho za Baba yake  huko Dar Juzi.


Mchumba wa askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), aliyeuawa kwa kupigwa risasi akiwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Luteni Asia Hussein aliyekuwa naye kabla ya kuuawa mchumba wake amesema, marehemu alimwomba amwombee arudi salama kutoka kwenye mapigano.
Pia, alisema kauli hiyo ndiyo ya mwisho kuisikia kutoka kinywani mwa mchumba wake huyo aliitoa baada ya kutolewa amri ya kijeshi kwamba anatakiwa kwenda kuwasaidia wenzake waliokuwa kwenye mapigano na askari wa waasi wa M23.
Askari huyo wa(JWTZ), Luteni Rajab Ahmed Mlima, aliuawa akiwa kwenye uwanja wa mapambano na vikosi vya askari wa waasi wa M23 katika milima ya Gavana, karibu na Goma, DRC wakati akitekeleza jukumu la ulinzi wa amani.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili jana nyumbani kwake, Luteni Asia alisema, “Ninachokumbuka walitakiwa kwenda kuwasaidia wenzao waliokuwa kwenye mapigano kwa muda mrefu, tayari walikuwa wamezidiwa nguvu na askari wa waasi wa M23, ukweli hali ilikuwa mbaya na mimi nilimkataza asiende kwa kuhofia usalama wake,” alisema Luteni Asia huku akibubujikwa machozi.
Alisema wakati akimsihi asiende alimjibu kwamba ni lazima aende kuwasaidia wenzao, kwani kazi waliyotumwa kuifanya ni pamoja na hiyo hivyo asingeweza kuacha kwenda.
Aidha, Luteni Hussein alibainisha kuwa baada ya kwenda kutoa msaada na kufanikiwa kuwadhibiti waasi, muda mfupi baadaye alipata taarifa kuwa Luteni Mlima amefariki kwa kupigwa risasi jambo lililomshtua kiasi cha kuishiwa nguvu kabisa.Kusoma zaidi bofya
Alisema kwa kuwa kazi ya Mungu haina makosa, yeye anamwombea huko aliko apumzike kwa amani kwani amefariki akiwa anawatetea wananchi wa DRC na kuiwakilisha nchi yake.
Mipango ya harusi
Akielezea mipango yao ya harusi, Luteni Asia alisema Desemba 28, mwaka huu walipanga kufunga ndoa na kwamba taratibu zote zilikuwa zimekamilika ikiwa pamoja kutolewa mahari.
“Kwa kweli jambo linalo niuma sana na siwezi kusahau ni kwamba, tulikuwa tumebakiza muda mfupi tufunge ndoa na kila kitu kilikuwa kimeshakamilika hadi ukumbi wa kufanyia sherehe ya harusi yetu tulishaulipia,” alisema Luteni Hussein huku akibubujikwa na machozi.

Portrait of the fallen soldier Lt. Rajab Ahmed Mlima


  He lost his life for the values of the United Nations, for protecting civilians, for defending human rights, for fighting for the benefit of the Democratic Republic of the Congo."
Message from UN Secretary-General Ban Ki-moon's Special Representative for the Democratic Republic of the Congo travelled to Kiwanja from Goma on Monday (28 Oct) to officiate a memorial service for the Tanzanian soldier killed recently in Rutshuru. Kiwanja is situated 70 km north of Goma, the capital of the North Kivu province of the DRC. Martin Kobler, who is also the Head of the United Nations Organization Stabilization Mission in the Democratic Republic of the Congo (MONUSCO) presided over the ceremony. He paid tribute to the fallen soldier, Lt. Rajab Ahmed Mlima, who died in line of duty while fighting the M23 rebels. Several other soldiers were also injured in the fight. The soldier from the Tanzanian Special Forces was part of the Intervention Force Brigade (IFB) that was formed to disarm armed groups in the North Kivu province. Fighting between the Congolese army the FARDC and M23 rebels resumed last week in the area known as Kibumba, 20 km from Goma. In recent days, the M23 rebels have lost key positions like Kibumba, Kiwanja, Rutshuru and Rumangabo.

Thursday, October 31, 2013

LIJUE SOKO LA HISA LA DAR

TUSHIRIKIANE TULITANGAZE SOKO LETU LA HISA Jifunze kuwa mwekezaji wa soko la Hisa Wasiklize mameneja mbali mbali wa soko la Hisa la Dar

  Watanzania tunaweza !
MAWAKALA WALIOSAJILIWA: Benki Kuu ya Tanzania imesajili mabenki na makampuni yafuatayo kufanya kazi za uwakala kwa wawekezaji . • Akiba Commercial Bank Ltd. • Citibank (T) Ltd. • CRDB Bank Ltd. • Diamond Trust Bank (T) Ltd. • Eurafrican Bank (T) Ltd. • Exim Bank (T) Ltd. • Habib African Bank Ltd. • International Bank of Malaysia (T) Ltd. • Kenya Commercial Bank (T) Ltd. • NBC Limited • NMB Ltd. • Stanbic Bank (T) Limited. • Standard Chartered Bank Ltd. • Orbit Securities Co. Ltd. • Rasilimali Limited • Solomon Securities Ltd. • Core Securities Ltd. • Tanzania Securities Ltd. • Vertex International Securities.

Saturday, October 26, 2013

BOOKS PUSH PROJECT YA JUMUIYA YA WATANZANIA DMV YAPATA MSAADA WA VITABU


Rais Wa Jumuiya ya Watanzania DMV Iddi Sandaly wa pili kulia pamoja na Muweka Hazina wa Jumuiya Genesa Malasy(Wa kwanza kulia) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Watanzania DMV Amos Cherehani (wa kwanza toka kushoto) katika picha ya pamoja na Mwalimu wa School Without Walls ya Wshington DC, Edwrd Ismail (wa pili toka Kushoto) Na Mwanafunzi wa Schoool Without Walls katika picha ya pamoja siku ya Ijumaa Oct 25, 2013 siku Jumuiya ilopopata msaada wa vitabu toka shule hiyo, vitabu vitakavyopelekwa Tanzania chini ya mpango mpya wa Jumuiya ya Watanzania DMV  na School Without Walls unaoitwa "BOOKS PUSH PROJECT". Vitabu vitasambazwa kwenye shule mbalimbali zikiwemo za msingi, Sekondari na Vyuo Vikuu. 

Uongozi unawajulisha watanzania wote kuwa watakuwa wakikusanya vitabu vya Sayansi vyote, Uhasibu, Biashara, Hisabati, English na Dictionaries pamoja na Vitabu vya watoto . 
Kwa Maelezo zaidi tuma email: info@watanzaniadmv.org or http://www.watanzaniadmv.org/contact.asp
Ukusanyaji ni Kila siku ya Jumamosi 3:00PM- 5PM
3621 CAMPUS DRIVE, COLLEGE PARK, MARYLAND




Elias Mshana (Didi Vava) na Simba Sakapala , wa kwanza na pili kutoka kulia Watanzania wa DMV ambao walijitolea kwenda kuwasaidi Viongozi wa Jumuiya kwenye kukusanya vitabu hivyo.